30 kwa 30 (au 30x30) ni mpango wa Dunia nzima kwa serikali kutenga 30% ya ardhi na bahari kama maeneo yanayotunzwa ufikapo mwaka 2030.[1][2]
Lengo lilipendekezwa na makala ya 2019 katika Science Advances, ikionesha hitaji la kupanua juhudi za kuhifadhi mazingira kupunguza mabadiliko ya tabianchi.[3][4] Ilizinduliwa na High Ambition Coalition mwaka 2020, Zaidi ya mataifa 50 yalikubaliana na mpango huu mnamo Januari 2021[5] ambao ulipanuliwa kwa zaidi ya nchi 70 mnamo Oktoba mwaka huohuo. 30 kwa 30 ilitangazwa kwenye kikao cha COP15 cha Convention on Biological Diversity.[6] Hii ilihusisha G7[7] na Umoja wa Ulaya.